Languages - Swahili

Karibu Victorian Multicultural Commission
Victorian Multicultural Commission (VMC) ni mamlaka ya kujitegemea kisheria yenye wajibu wa kutekeleza maelewano na kuhamasisha ushiriki wa jumuiya za Victoria zenye utamaduni ,lugha na dini tofauti katika masuala yote ya maisha hapa Victoria.
Malengo na kazi za Commission, kama zilivyo kwenye Multicultural Victoria Act 2004, ni pamoja na kusaidia na kuwezesha jumuiya, kuhamasisha umoja na maelewano, na kusherehekea tofauti za kiutamaduni hapa Victoria.
Uwezo mkubwa wa VMC ni pamoja na:

  • Mfuko wa Programu ya Jumuiya – huweza kutoa fedha kwa kundi la jumuiya katika makundi saba: Kusaidia utaratibu wa chama, raia waliostaafu,Majengo na Vifaa,Sherehe na Utendaji, kuimarisha jumuiya zenye Tamaduni Nyingi, Utendaji wa Imani nyinginezo/Imani kati ya, na Programu za Elimu.
  • Fedha za Kuboresha kituo cha utamaduni - kuwekeza $10 milioni kwa kipindi cha miaka mitatu ili kufanikisha uwepo wa vituo vitatu vya muda mrefu na taswira kubwa za utamaduni hapa Melbourne: Little Bourke, Lonsdale and Lygon Streets.
  • Kuhamasisha na Kuanzisha Mapatano - Ni moja ya miradi unaolenga kudumisha na kuhakikisha sifa nzuri ya Victoria kama jamii inayokaribisha na kupatana na watu. Ikiwa ni pamoja na Wiki ya Tofauti za Utamaduni, Kampeni inayohusu Sisi Wote, Utendaji wa Imani nyinginezo na Imani kati ya na ushirikishi wa vijana
  • kakati wa Huduma za Lugha – Kusimamia utumiaji unaotakiwa wa watafsiri ili kuwezesha kupata huduma za serikali na kuendeleza ubora na wingi wa watafsiri wa Victoria.
  • Programu inayohusu wakimbizi - Ikishirikiana na mashirika makuu na jumuiya za wakimbizi programu hii ya jimbo lote hutoa misaada muhimu kwa wakimbizi waliowasili hivi karibuni hapa Victoria na wale waliokuja kwa hisani za kibinadamu.

VMC pia husimamia mlolongo wa kamati za ushauri pamoja na viongozi wa jumuiya, viongozi wa dini/imani, serikali za eneo na vijana ili kuamua mahitaji ya jumuiya za Victoria zenye utamaduni ,lugha na dini tofauti.
Habari zaidi zilizochapishwa zinapatikana kwa lugha ya [KISWAHILI]:

Ili kujiunga na vikundi katika eneo unaloishi au jumuiya angalia Community Resources Directory na utafute kwa eneo au kwa kabila au kikundi cha utamaduni.

Last Updated on Monday, 30 November 2009 14:54
PDF Print E-mail
 

Events Calendar

  • 27 May

    Reconciliation Week - free activities

    more >
  • 26 May

    International Dinner

    more >
  • 26 May

    Africa Day 2012

    more >
  • 25 May

    La Fiera Italian Festival

    more >
find more events here >